Msanii Recie Officiel amewashangaza mashabiki wake baada ya kutangaza rasmi kwamba anafunga ukurasa wa safari yake ya muziki.
Kupitia ujumbe aliowashirikisha mashabiki wake, Recie amewashukuru kwa upendo, sapoti na uaminifu waliomuonyesha tangu mwanzo wa safari yake ya kimuziki.
“Leo safari yangu ya muziki imefika mwisho. Kila hatua, kila wimbo na kila wakati tuliopitia pamoja, yote yaliwezekana kwa sababu ya sapoti na upendo wenu.”
Recie ameendelea kueleza kuwa kumbukumbu zote alizopata pamoja na mashabiki wake zitabaki moyoni mwake daima. Pia amewashukuru kwa kumuamini, kusimama naye na kumpa nguvu katika kila hatua ya safari yake.
Tangazo hili limeibua hisia mbalimbali kwa mashabiki wake, ambao sasa wanasubiri kujua zaidi kuhusu sababu iliyomfanya msanii huyo kufanya uamuzi huo.
Je, huu ndio mwisho wa safari ya Recie Officiel kwenye muziki, au ni mwanzo wa ukurasa mpya? 🥺🕊️










